Saturday, 22 August 2015

ALLAH IS GREAT!!!

🌄🌻🌄🌻🌄🌻🌄🌻🌄 FADHILA ZA RAKAA ✌ MBILI ZA SUNNA KABLA YA SALA YA ALFAJIR🌄

 ➡Imesimuliwa👂 na Bibi Aisha (radhwiya Allahu anha) amesema

 👉Mtume(swalla Allahu alayhi wasallam)

 " Rakaa mbili✌ za sunna kabla ya sala ya alfajiri🌄 ni bora kuliko dunia🌎 na vilivyomo ndani yake"
 👉Imepokelewa na Imam Muslim na Tirmidhi.👐

 ❗Subhanallah dunia🌏 ina mazuri mangapi❓ ambayo wanaadamu wameyapa thamani. mali na fedha,💰💴 mashamba, wanawake👩🙎 na watoto👶👦👱, vipando na vyenginevyo, vyote hivyo havina thamani mbele ya rakaa mbili✌ za kabla ya sala ya alfajiri.🌄

 ❓Wangapi wanalielewa hili❓

 👉Kwani inasimuliwa👂 na Bibi Aisha kuwa:

 👉” Hakuna swala yoyote ya Sunna ambayo Mtume alikua akiitilia mkazo zaidi kama rakaa mbili✌ kabla ya sala ya alfajiri”🌄
 Imepokelewa na Bukhari na Muslim.

 👉Ni wachache wanaoswali alfajiri🌄 na ni wachache katika wanaoswali alfajiri wanaswali rakaa mbili✌ kabla ya alfajiri🌄.

 Ndugu zangu rakaa mbili✌ hizi zina thamani kubwa mpaka kulinganishwa na 🌏dunia na vilivyomo ndani yake. Na tujiulize duniani 🌍 kuna majumba mangapi 🏰🏯❓  Magari mangapi🚗🚘❓
 Dhahabu🔶 na almasi💎 na madini mengine kiasi gani❓❓

👉 Vyote hivyo vimepitwa na rakaa mbili✌ kabla ya sala ya alfajiri🌄 ambazo hazizidi dakika 5.👊

 Na imesimuliwa👂 kuwa Mtume alikua akisoma sura ndogo📖 ndani ya rakaa ✌2 hizi. 👉Tujitahidini kuweza kuswali sala ya Alfajiri🌄 na pia kutekeleza sunna hii ya rakaa 2✌ kabla ya sala ya alfajiri.🌄

 👐ALLAH atuwafikishe katika kheri hizi. 👐AMIIN!!!
 Wa-ALLAHU ‘aalam. 🌴🌄TUELEKEZANE PEPONI🌴🌄                            🌄🌻🌄🌻🌄🌻🌄🌻 Jee! unaifahamu siku inayoitwa YAUMA TUBLA SARAAIRU? ni siku ambayo zitafichuka siri za WANAADAM Woote, ni siku ambayo ARDH itasema, Mikono itasema, na Miguu itatoa ushahidi kama alivyosema Allah(s.w) WATUKALLIMUNAA AIDIIHIM WATASH-HADU ARJULUHUM BIMAAKAANU YAKSIBUUN. Huo ni ukumbusho, watumie wengine ili iwe sadaka kwetu lnshaallah. ni hasara kama utaacha kutoa sadaka hii kwa Waisilamu wenzako ambao hawajui au wamesahau ujumbe huu.

No comments:

Post a Comment

Ar~Razzaq

Allah is Ar-Razzaq. It is He Who is the Provider and Bestower of sustenance. He provides and delivers His creations with wha...